Nangatai
Vipimo
Unga wa ngano 2 - 2 ¼ Vikombe
Siagi 1 ½ Kikombe
Sukari 1 Kikombe
Yai 1
Vanilla Tone moja
Baking Powder 2 Vijiko vya supu
Chumvi Kiasi kidogo (pinch)
Unga wa Kastadi 2 Vijiko vya supu
Namna ya kutayarisha na kupika
1. Changanya vitu vyote isipokuwa unga.
2.
Tia unga kidogo kidogo mpaka mchanganyiko uwe sawa.3. Kisha fanya duara ndogo ndogo uzipange kwenye treya na utie rangi katikati.
4. Halafu zichome katika moto wa 300°F kwa muda wa dakika 20 - 25 na zisiwe browni .
5. Kisha panga kwenye sahani tayari kuliwa na chai.
Ahsante bwana kwa kutujuza elimu ya mapishi
ReplyDeleteAsante
ReplyDelete